KOCHA msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa wanajenga kikosi imara kitakachokuwa na uwezo wa kucheza dakika 120 katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara.
Pamoja na kuanza msimu kibabe, chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Mserbia Zlatko Krmpotic, wachezaji wa timu hiyo wameoneka kutohimili kucheza dakika 90
Mwambusi alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga baada ya Krmpotic kutimuliwa hivi karibuni ambaye mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi kuiongoza timu hiyo ilicheza mechi ya kirafi ki dhidi ya Mwadui FC.
Yanga katika mchezo huo dhidi ya Mwadui walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mghana Michael Sarpong, kabla ya kupokea pasi ya kiungo mshambuliaji Carlos Fernandes ‘Carlinhos’.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwambusi alisema amefurahishwa na viwango vya wachezaji walivyovionyesha kwenye mchezo huo dhidi ya Mwadui huku akipanga kuanza programu ya wiki tatu itakayokuwa na fi tinesi pekee.
Kocha huyo alisema kuwa lengo la kuwapa program hiyo ya fi tinesi ni kuwafanya wachezaji kucheza katika viwango vya juu kwa kwa kuanzia dakika 120 za mchezo.
“Tulicheza vizuri pamoja na kuwa ulikuwa ni mchezo wa kirafi ki tu na tulipaswa kumpa nafasi kila mchezaji.
Yapo mapungufu tuliyoyaona kama benchi la ufundi ambayo tumepanga kuyafanyia kazi.“Ninataka kuona wachezaji wanakuwa na uwezo wa kucheza dakika zote 90 hadi 120 bila kuchoka, lakini kwa kiwango na spidi ileile.
Nadhani baada ya wiki tatu hivi vyote tunavyovifanyia kazi vitaanza kuonekana na kutoa matokeo mazuri zaidi,” alisema Mwambusi.