Korea Kaskazini kuweka hadharani silaha zake katika gwaride la Jeshi



Korea kaskazini inajiandaa kwa kile kinachotarajiwa kuwa gwaride kubwa la kijeshi katika historia yake.


Maelfu ya wanajeshi wamefanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inafana mbele ya rais Kim jong-un.


Hafla hiyo hutumika kama onesho la uwezo wa kijeshi huku raia watiifu wakiendelea kumuheshimu kiongozi wao huku makosa yakiwa hayawezi kukubalika.


Taifa hilo halijaonyesha makombora yake ya masafa marefu katika magwaride yake tangu rais Donald Trump na Kim Jong-un walipofanya mkutano wao wa kwanza mnamo 2018.


Lakini gwaride hizi pia zinaweza kuwa njia ya sehemu ya uchokozi . Nafasi ya kuonyesha makombora na silaha mpya licha ya taifa hilo kuwa chini ya vikwazo vikali vya kiuchumi.


Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalivunjika huko Hanoi mnamo Februari iliyopita bila makubaliano na Korea Kaskazini imeendelea kufanyia majaribio makombora kadhaa ya masafa mafupi.


Hafla hii, inayofanyika tarehe 10 Oktoba, ili kuadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwa Chama cha Wafanyakazi inajiri wiki chache kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani.


Je tunauliza Korea Kaskazini itatumia kutoa hoja na kudhibitisha kuwa bado ina silaha zenye uwezo wa kuishambulia Marekani?


Silaha mpya katika gwaride

Kwa kweli itakuwa hafla kubwa, kulingana na mhariri mkuu wa tovuti ya Daily NK, wavuti ulio na makao makuu yake mjini Seoul na ambao unategemea wafadhili huko Korea Kaskazini.


Lee Sang Yong aliniambia kuwa mapema Machi, Pyongyang ilikuwa imeamuru kuwa na wanajeshi 32,000 katika gwaride hilo. Gwaride hilo limekuwa kubwa sana hai ya kwamba eneo ambalo hafla hiyo hufanyika imelazimika kupanuliwaWanajeshi wa jeshi la Korea kaskazini


Wanajeshi wa jeshi la Korea kaskazini

”Uwanja wa ndege wa Pyongyang Mirim sasa una barabara mbili mpya na majengo 10 mapya. Kwa hivyo, nadhani kuna uwezekano kwamba tutaona Makombora yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine [ICBMs] au makombora yanayoweza kurushwa kutoka kwa Manowari [SLBMs] yakionyeshwa kwenye gwaride wakati huu,” alisema


”Pia, wanafunzi na watafiti 600 kutoka Chuo Kikuu cha Kim Il-sung pia watashiriki. Hii sio idadi isiyo na maana. Chuo kikuu hiki ndicho wanachotumia kukuza talanta mpya za uundaji wa makombora. Kwa kuwaleta kwenye gwaride au kuwaweka kwenye onyesho, Korea Kaskazini inaweza kuwa inajaribu kujivuna na kutaka kuheshimiwa kuhusu talanta walio nayo ya uundaji wa makombora “


Jeongmin Kim, mchambuzi wa NK News, anasema Korea Kaskazini haitumii kila hafla hizi kila wakati kujionesha kwa ulimwengu.


“Lazima tukumbuke kwamba mara nyingi – kwa taifa linalotawaliwa kidikteta – inabidi kila wakati uthibitishe uhalali wa utawala wako kwa raia .


“Kwa hivyo Oktoba 10 pia itakusudia kufanya hivyo kabisa: kujaribu kuwaonyesha watu wake, gwaride zenye kupendeza na kauli mbiu za kueneza uwongo, kwamba” wanaendelea sawa “, licha ya yote ambayo yamekuwa yakiendelea mwaka huu.


“Kwa kweli, mifano inaelezea uwezekano wa Kim Jong-un au maafisa wengine wa ngazi ya juu kutoa hotuba ambayo inaweza kuhusisha ujumbe fulani unaolenga ulimwengu, kama vile hatusubiri kuondolewa vikwazo tena na kuzingatia ‘kujitegemea’. “


Korea Kaskazini imejitenga na ulimwengu


Wakati wengine wanatazama makombora mapya kwenye maonyesho, kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu ustawi wa watu milioni 25 wa Korea Kaskazini.


Mwaka wa 2020 umekuwa mwaka mbaya kwa nchi nyingi, lakini kwa Korea Kaskazini inawezekana umekuwa mbaya zaidi


“Nasikia kuna ongezeko la idadi ya watoto yatima na wasio na makazi mitaani katika maeneo ya kaskazini mwaka huu,” Lee Sang Yong alisema.


“Ingawa hatuwezi hata kufikiria hapa Korea Kusini – kuna watu Kaskazini ambao wanakufa na njaa.”


Taifa hilo lilifunga mipaka mnamo mwezi Januari kuzuia kuzuka kwa Covid 19 kuenea kutoka taifa jirani la China.


Mamlaka imeripotiwa kutoa maagizo ya kumpiga risasi na kumuua mtu yeyeote katika eneo la mpakani na kuweka zuio ili kumzuia mtu yeyote anayeingia nchini humo.


Vyanzo vya kidiplomasia viliniambia mapema mwaka huu kwamba PPE na vifaa vingine muhimu vya matibabu, pamoja na chanjo, vilikuwa vimejaa mpakani na China, vikiwa haviwezi kuingia nchini humo.


Korea Kaskazini inadai kwamba haina kesi za Covid-19, lakini Kim Jong-un anaendelea kufanya mikutano ya kiwango cha juu kuhakikisha vizuizi vikali vinasalia.


Raia wa Korea Kaskazini sasa wametengwa na ulimwengu wa nje zaidi ya awali. Hata harakati za usafiri kutoka jimbo moja hadi jingine zimeathirika.Silaha za Korea kaskzini


Makombora yanayoweza kufika Marekani

Katika kipindi cha mwaka 2017, Korea Kaskazini ilijaribu makombora kadhaa kuonesha maendeleo ya haraka ya teknolojia yake ya kijeshi.


Hwasong-12 ilifikiriwa kuwa inaweza kufikia umbali wa kilomita 4,500 (maili 2,800), ikiiweka ngome ya jeshi la Marekani kwenye kisiwa cha Pacific cha Guam katika umbali mzuri wa kuipiga


Baadaye, Hwasong-14 ilionesha uwezo mkubwa zaidi huku tafiti nyingine zikionesha kwamba inaweza kusafiri hadi kilomita 10,000 ikiwa itarushwa anga za juu.


Hii ingeipa Pyongyang kombora lake la kwanza (ICBM), linaloweza kufikia New York.


Hatimaye, Hwasong-15 ilijaribiwa, ikifika umbali wa wastani wa kilomita 4,500 – mara 10 zaidi kuliko Kituo cha Anga cha Kimataifa.


Kombora likiwa limefyatuliwa linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 13,000, na kuiweka kwenye shabbaha eneo la bara la nchi ya Marekani.


Hatahivyo, mashaka yanabaki ikiwa makombora haya yanaweza kufanikiwa kubeba silaha ya vita kwa umbali kama huo, na ikiwa Korea Kaskazini ina utaalam wa kufikia lengo.


Mnamo mwaka 2019, Korea Kaskazini ilifanya majaribio kadhaa ya kombora la masafa mafupi, ambayo iliongezeka mnamo Julai na Agosti kwa kile ilichokiita “maonyo” kwa Marekani na Korea Kusini kuhusu mazoezi yao ya kijeshi


Kisha mnamo mwezi Oktoba, Pyongyang ilionekana kuwa na uwezo mpya ilipojaribu kombora linaloweza kurusha kutoka kwenye nyambizi.


Kwa nadharia, kuweza kuzindua kombora lenye vifaa vya nyuklia kutoka kwenye nyambizi huongeza uwezo wa Korea Kaskazini wa kushambulia . Tishio hilo linakabiliwa na meli za zamani na ndogo za nyambizi za nchi hiyo, ambazo zinaweza kufanya safari ya kwenda moja kwa moja hadi Hawaii.


Mafanikio dhahiri ya majaribio haya yote yameibua maswali kuhusu jinsi mpango wa makombora wa Korea Kaskazini ulivyoimarika haraka sana. Waangalizi wanaamini Pyongyang inaweza kuwa imepata injini zinazofanya kazi kwa kiwango cha juu kutoka kwa mitandao haramu nchini Urusi na Ukraine.Kombora la Hwasong 14


Korea Kaskazini imeendelea na uboreshaji wa mpango wa silaha, ikizindua majaribio ya kombora mwanzoni mwa mwaka huu.


Mnamo mwezi Julai, kiongozi wake Kim Jong-un alisema Pyongyang ilitengeneza silaha za nyuklia ili kupata “nguvu”, na kuongeza kuwa nchi hiyo sasa “ina uwezo wa kujilinda”.


Mabomu ya nyuklia


Mnamo tarehe 3 Septemba 2017 Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake kubwa zaidi la nyuklia hadi sasa, katika eneo lake la majaribio la Punggye-ri.Ramani inayoonesha majaribio ya nyukilia


Idara ya Intelijensia ya jeshi la Marekani inaamini kuwa Korea Kaskazini imefanikiwa kutumia silaha ya nyukilia kutosha ndani ya kombora.


Mwezi Aprili mwaka 2018 Korea Kaskazini ilitangaza kusitisha majaribio zaidi ya nyukilia kwa sababu uwezo wake ulikuwa “umethibitishwa”.


Pyongyang pia alisema basi kwamba itaharibu vinu vyake vyote vya nyuklia.


Mamilioni ya wanajeshi


Korea Kaskazini ina moja wapo ya vikosi vikubwa ulimwenguni – ikiwa na zaidi ya wanajeshi milioni moja na wa akiba wanaokadiriwa kuwa milioni tano.


Vifaa vyake vingi ni vya zamani , lakini vikosi vyake vya kawaida bado vinaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa Korea Kusini wakati wa vita.


Korea Kaskazini pia ina karibu vikosi 200,000 maalum ambavyo vinaweza kutarajiwa kupenya Kusini iwapo kutatokea mzozo wowote.


Wanaweza kutumia mtandao wa siri-siri wa mifumo ya chini kwa chini 20-25 iliyo katika eneo la Demilitarized (DMZ) – eneo la mpaka – linaloibuka nyuma ya safu za mbele za Korea Kusini na Marekani.Majeshiwhite space


Tishio zaidi linatokana na maelfu ya vipande vya silaha za Korea Kaskazini na virusha roketi vilivyowekwa mpakani. Nguvu yake inaweza kuitikisa Korea Kusini, pamoja na mji mkuu wa Seoul, ambao uko chini ya umbali wa kilomita 60 kutoka eneo hilo


Silaha za kemikali pia zinaweza kutumika. Mnamo mwaka 2012 serikali ya Korea Kusini ilitathimini kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwa na kati ya tani 2,500 na 5,000 za silaha za kemikali, ambayo inaweza kuwa moja wapo ya hifadhi kubwa duniani.


Vikosi vya Marekani Korea Kusini na katika eneo la ukanda


Majeshi ya Marekani yamekuwa Rasi ya Korea tangu Vita vya Korea. Leo, Korea Kusini ni ya tatu kwa kuwa na kikosi kikubwa cha jeshi la Marekani ulimwenguni.


Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mkakati (IISS) kuna wanajeshi 28,000 wa Marekani walio Korea Kusini wakiwemo karibu wafanyikazi wa jeshi la anga 9,000. Kwa kuongezea, Marekani ina vifaru 300 vya M1 Abrams na magari ya kivita yaliyopelekwa.Silaha ya B-1B Spirit bomber ya Marekani


Washington pia imeweka mfumo wake wa mfumo wa kizuizi cha makombora ya THAAD huko Seongju huko Korea Kusini, ambaoo ungetumika kuzuia makombora ya masafa mafupi na ya kati ya Korea Kaskazini wakati wa vita.


Kikanda,Japan ina vikosi vingi vya Marekani kuliko taifa lingine lolote, na wengine 47,050 wamepelekwa, kulingana na IISS, wengi wao wakiwa wafanyikazi wa majini. Pia ina wabebaji wa ndege walio Japani.


Pia kuna vikosi muhimu vya Marekani kwenye kisiwa cha Pasifiki cha Guam, ambacho wakati mwingine huelezewa kama “mbebaji wa ndege wa kudumu”.


Korea Kaskazini hapo awali ilitishia kufyatua makombora kwenye maji karibu na Guam.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad