LIONEL Messi amekuwa ni nembo ya Klabu ya Barcelona kwa muda mrefu tangu kuondoka kwa Ronaldinho mwaka 2008, lakini kumbe wapinzani wao wa jadi, Real Madrid, waliwahi kutuma ofa ya kutaka kumsajili Rais wa Madrid, Florentino Perez alifanya mpango huo mwaka 2013 lakini dili likawa gumu licha ya kuwa alikuwa tayari kumwaga fedha kumsajili Messi.
“Maombi ya usajili ya Florentino Perez yaliwasilishwa mwaka 2013 na aliweka mezani euro 250m (Sh bilioni 673) ili kumsajili Messi.“Fedha hizo awali zilipangwa kutumika katika mradi wa Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa ajili ya maboresho.
“Lakini suala la kumsajili Messi lilikuwa ni muhimu na ndiyo maana fedha hizo zikatengwa maalum,” kilieleza chanzo cha habari mara baada ya taarifa hizo za dau la usajili kufika kwa Messi, akatoa jibu moja tu: “Siwezi kwenda Real Madrid, mnapoteza muda wenu tu.
”Baada ya jibu hilo ikabidi Madrid wajiongeze wenyewe na kuendelea na mambo yao mengine.Mbali na hapo Inter Milan chini ya bosi wao Massimo Moratti ilikuwa ikimuhitaji Messi kama ilivyokuwa kwa Chelsea, Paris Saint-Germain na Manchester City lakini zote hazikupata kitu.
Mkataba wa Messi wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 2021, na tayari Messi mwenyewe ameshaonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo.