Lionel Messi alikubali kujiunga Chelsea



Mwaka 2014, Jose Mourinho alimshawishi mchezaji bora duniani, Lionel Messi kujiunga na Chelsea akitokea Barcelona

Mara kadhaa Messi alikuwa akipokea simu kutoka kwa Mourinho zilizokuwa zikimshawishi kutua Stamford Bridge wakati ambao Chelsea na Real Madrid walikuwa wapo tayari kutoa paundi milioni 225 kwaajili ya uhamisho wa nyota huyo huku miamba ya soka ya England ikiwa tayari kumpatia mshahara wa paundi milioni moja kwa wiki hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari, Di Marzio


Mchawi huyo wa soka mwenye umri wa miaka 33 mara kadhaa amejaribu kutaka kuonda La Liga hata siku za hivi karibuni mwezi Agosti alionyesha nia hiyo wakati ambapo dau la yeye kung’olewa Barcelona lilipowekwa wazi kuwa euro milioni 700.


Lakini mwaka 2014, Chelsea walikuwa wapo tayari kutoa euro milioni 250 kama ‘release clause’ na kumpatia Muargentina huyo paundi milioni 50 kwa msimu na pengine angevunja rekodi ya usajili kwa kipindi hicho.


Mazungumzo hayo yalikuja kushindikana baada ya serikali ya Hispania kuibuka na kuifungulia kesi familia ya Messi kuhusiana na ukwepaji kodi uliyotokea mwaka 2013.


Katika kitabu chake cha hivi karibuni cha Grand Hotel Calciomercato, ‘diary’ ya habari zisizojulikana katika dirisha la usajili, Di Marzio anafunua njia zote ambazo Mourinho alivyokuwa akiwasiliana na Messi ili kuhakikisha anatua Chelsea.


Mpango huo uliyowahusisha baba yake mzazi, wakala wake Jorge na aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake Deco uliyayuka mithili ya povu la sabuni linapopasuka na kutoweka katika hewa licha ya kuwa masharti binafsi baina Messi na Chelsea kukubaliwa.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad