Maafa ya maporomoko ya ardhi Pakistan: 16 wafariki

 


Watu 16 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana mafaa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokewa katika maeneo ya Gilgit-Baltistan nchini Pakistan.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Pakistan, iliarifiwa kuwa basi moja dogo lilididimia chini na kufunikwa na ardhi wakati lilipokuwa likisafiri kwenye njia ya mlima kutoka Rawalpindi kuelekea Skardu.


Kamishna msaidizi wa idara ya usalama ya Rondu iliyoko eneo la Gilgit-Baltistan, Miraj Alam, alibainisha kufariki kwa watu 16 kwenye maafa ya maporomoko ya ardhi.


Amal pia alibaini kukamilishwa kwa shughuli za utafutaji na uokoaji kwenye eneo la tukio.


Nchi ya Pakistan imekuwa ikikumbwa na maafa ya maporomoko ya ardhi mara kwa mara yanayosababishwa na mafuriko hasa kwenye maeneo ya milima na mabonde, kutokana na mvua za masika.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad