Maambukizi ya Corona yaongezeka kwa kasi Afrika




Visa vya maambukizi ya virusi vya corona vinaongezeka kwa kasi katika baadhi ya maeneo ya Afrika na serekali zinatakiwa kuchukua mikakati ya kukabiliana na wimbi la pili la maambukizi, kituo cha kukinga na kudhibiti magonjwa barani Afrika kimesema jana. Katika wiki nne zilizopita, visa vya maambukizi viliongezeka kwa asilimia 45 kwa wiki nchini Kenya, asilimia 19 nchini DRC na asilimia 8 nchini Mistri, kiongozi wa kituo hicho, John Nkengasong amesema. “Muda wa kujiandaa kwa wimbi la pili kwa kweli ni hivi sasa”, amesema, akizisihi serekali kutochoshwa na kuchukua hatua za kukinga. 


Bara la Afrika lenye watu billioni 1.3 lilifanikiwa kudhibiti janga la corona kuliko ilivyokua inatarajiwa, likiwa na asilimia ndogo ya vifo kuliko katika kanda nyingine, kutokana na hatua kali za kufunga shughuli zote zilizochukuliwa mwezi March. Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad