Maandamano yamefanyika nchini Georgia kwa ajili ya kuunga mkono operesheni iliyoanzishwa na jeshi la Azerbaijan kwa ajili ya kukomboa ardhi ya yao.
Waandamanaji walikusanyika katika mji wa Marneuli, na kudhihirisha wa kupinga uvamizi wa Nagorno-Karabakh uuliotekelezwa na Armenia, na kuliunga mkono jeshi la Azerbaijan.
Maandamano hayo yalijumuisha raia wa asili ya Azerbaijan, waatalam wa kisiasa wa Georgia, wasomi pamoja na wanahistoria.
Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba bendera za Uturuki na Azerbaijan, walitoa kaulimbiu inayosema, ‘‘Nagorno-Karabakh ni ya Azerbaijan.’’
Waandamanaji pia waliweka msisitizo Nagorno-Karabakh ipo chini ya uvamizi wa Armenia, na kutaka irejeshwe kwa Azerbaijan.
Wataalamu wa Georgia nao walibainisha kuwa ardhi ya Nagorno-Karabakh ni ya Azerbaijan na ni haki yao wanaostahili kuilinda mpaka mwisho. Hivyo basi Azerbaijan inastahili kuungwa mkono.
Baada ya maandamano hayo yaliyodumu kwa takriban masaa 2, vijana waliokuwa wamebeba bendera za nchi tatu walitoa kaulimbiu za "Karabakh itakuwa yetu" na "Mashahidi hawafi, Taifa lao haligawanyiki."
P