Machafuko mapya yazuka Lagos baada ya mauaji ya waandamanaji



Risasi zimerindima na gereza moja kuchomwa moto katika machafuko mapya mjini Lagos leo, baada ya kupigwa risasi waandamanaji kulikosababisha hasira za kimataifa. 

Polisi imesema washambuliaji walivamia kituo cha kuzuwilia wahalifu katika kiunga cha Ikoyi, katikati mwa Lagos, katika siku ya pili ya vurugu kwenye mji huo wenye wakaazi milioni 20, kufuatia ukandamizaji wa vikosi vya usalama dhidi ya maandamano. 


Rais Muhammadu Buhari, ambaye bado hajazungumzia ufyatuaji wa risasi katika maandamano hayo, ameitisha mkutano wa baraza la taifa la usalama leo, pamoja na waziri wake wa ulinzi na mkuu wa jeshi la polisi. 


Jeshi la Nigeria limekanusha ripoti kwamba wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji, na waziri wa polisi Muhammad Maigari, akisema katika mahojiano na shirika la utangazaji la BBC, kwamba wanajeshi hawakuamriwa kufyatulia risasi wandamanaji. 


Amnesty International imesema wanajeshi wa Nigeria waliwaua kwa kuwapiga risasi watu 12 siku ya Jumanne, huku jumla ya watu 56 wakifariki nchini kote tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya ukatili wa polisi na utawala mbaya, Oktoba 8.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad