Kijana aliyejulikana kwa jina la Casto Zakaria (28) mkazi wa Tukuyu Mbeya amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na kutobolewa macho tukio lililotokea katika kijiji cha Kisinga kata ya Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 24, 2020 ambapo kijana huyo aliyekuwa akifanya kazi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Moronga Makete chini ya kampuni ya CRSG, amefikwa na mauti huku taarifa za awali zikidai chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi
Wakazi wa kijiji hiki ambao wamefika eneo la tukio, wameeleza masikitiko yao kufuatia tukio hilo.
"Hili tukio kweli linasikitisha kwasababu ni tukio la kwanza kwenye kijiji hiki,na ukifuatila hata wazee wetu hamna mtu aliyewahi ua kwa kinyama namna hii"alisema Alisema Costantino swalo mkazi wa kijiji hicho.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga Bw. Mose Chaula amesema tukio hilo ni la kikatili na yeye anamiaka 7 madarakani lakini hajawahi shuhudia tukio la mauaji ya kikatili kama hilo
"mimi sasa hivi nina miaka saba kwenye uongozi sijawahi kutana na tukio kama hili,wito wangu kwa wananchi waachane na tabia hizi na kama kuna jambo linakuzidia uwezo jitahidi kuona uongozi wa kijiji na uongozi unaofuata"alisema Mose Chaula
Inadaiwa kwamba mke mdogo wa Marehemu aliyetajwa kwa jina la Adivera Msigwa alikutwa na mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mumewe Bw. Nolasco Msigwa nyumbani kwa marehemu huyo ambapo anatuhumiwa kutekeleza kitendo hicho cha mauaji na baadhi ya vitu vilivyokutwa nyumbani alipokuwa akiishi marehemu zikiwemo nguo na viatu vya kike vilipooneshwa kwa wananchi waliweza kuvitambua na kutaja.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy amefika eneo la tukio na kukemea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi na kupoteza uhai wa wenzao
"Ni tukio la kusikitisha sana kutoa uhai wa mwenzako kwa namna hii.hata kama ni kosa ukimkuta mwanaume yupo kwenye kifua cha mke wako,na hii inadhihirika mauaji haya ni wivu wa kimapenzi na kwa vielelezo vinavyosemekana viko ndani na jinsi alivyokutwa marehemu alikuwa anajaribu kujiokoa ametoka kama alivyozaliwa lakini kuna nguo za mwana mama ziko ndani pamoja na nguo za nyumba.Hiki ni kitendo cha kikatili mno,tuache kujichukulia sheria mkononi"alisema Veronika Kessy
Jeshi la polisi wilaya ya Makete linamshikilia mke wa mtuhumiwa aliyekutwa nyumbani kwa marehemu kwa hatua zaidi huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia baada ya kutekeleza mauaji hayo.