KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos, amejikuta katika wakati mgumu kutokana na kuteswa na Ugonjwa wa Malaria uliosababisha asiwemo katika sehemu ya kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara huko Kanda ya Ziwa.
Awali Carlinhos alikuwa nje ya uwanja kutokana na kupata majeraha ya kisigino katika mazoezi yaliyofanyika katika kambi yao iliyopo AVIC Town, Kigamboni jijini Dar.
Siku chache kabla ya kwenda Mwanza kucheza na KMC, kiungo huyo aliugua ghafl a Malaria ambayo inamtesa hadi sasa.
Akizungumza na Spoti Xtra, Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija, amesema, Carlinhos bado hayupo fi ti kutokana na kuendelea na matibabu ya malaria kulikomlazimu kutokuwa sehemu ya kikosi.
“Wachezaji wengine wapo fi ti isipokuwa Mapinduzi Balama ambaye anaendelea na matibabu pamoja na Carlinhos ambaye yeye bado anaendelea na dozi ya malaria na yupo Dar akiendelea kujiuguza.
“Kurudi kwake ku-nategemea na jinsi atakap-opata nafuu kwa mapen-zi ya Mungu,” alisema Mngazija.