Mamlaka huko Mali imetangaza kuachiliwa huru kwa wanasiasa kadhaa na wanajeshi waliokamatwa wakati wa mapinduzi ya Agosti.
Walioachiliwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Boubou Cissé.
Taarifa rasmi imeonesha kwamba waliokamatwa bado watasubiri uamuzi wa mahakama ikiwa kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.
Jumatatu, serikali ya mpito ilitangaza baraza jipya la mawaziri ambapo wanajeshi waliopanga mapinduzi walikabidhiwa nafasi muhimu serikalini ikiwemo ulinzi, usalama, utawala wa mipaka na maridhiano ya kitaifa.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imeiondolea Mali vikwazo, na kutambua kile ilichokitaja kama kupigwa kwa hatua muhimu kuelekea kwenye utaratibu wa kikatiba