Mambo matano ya kufanya kuhusu ndugu baada ya kuoa



1. Kama inawezekana hakikisha unaishi mbali na ndugu zako; Mwanaume unatakiwa kujua kuwa ukishaoa unatengeneza familia yako, ndugu zako ni familia ya Baba yako, kama unataka ndoa yako kusimama basi ishi mbali na ndugu zako, muwe mnasalimiana lakini si kulala na kuamka sehemu mmoja. Ishi nao tu kama ni lazima kuishi nao hasa wale wadogo, wale wakubwa wasaidie wakiwa kwao la sivyo ndoa yako itayumba. 


2. Mke ni wakwako, usiruhusu ndugu zako kumchezea wanavyotaka; Kamwe usiruhusu ndugu yako kumtukana mke wako, hata kama kakosea dili naye wewe ni wako, usiruhusu ndugu zako kumpangia kitu mke wako, kumtuma tuma na chochote kile, mambo ya hatutaki mke wako afanye kazi, sijui mke wako anatakiwa kukaa na Mama na mengine mengi upange wewe na si ndugu, usiwape kauli ndugu zako juu ya mke wako. 


3. Yule dada yako aliyeachika msaidie akiwa huko huko; Kuna ule mwezi wa kwanza katoka kwa mume wake, labda kapigwa, absi huo unatosha, baada ya hapo mtafutie kachumba hat aka elfu mbili akae na mwanae umsiadie huko huko. Huyo mtu ana hasira ya kuachwa, anachukia kuona wewe unamdekeza mke wako wakati yeye alikua anapigwa kila siku, lazima ataona wivu na atakuharibia ndoa yako, unampenda lakini ya kwake yalishamshinda usiruhusu akuharibie na yako. 


4. Unachuma mali kwaajili ya wanao hakuna mtu atawapenda wanao zaidi ya mke wako; Kama unadhani kuwa kuna mtu atawapenda wanao kuliko Mama yao basi umekosea, muangalie Mama yako na mlinganishe na Shangazi zako na ndugu wengine wa Baba, kama unampenda Mama yako basi jua kuwa mkeo Ndiyo Mama wa wanao, muamini yeye na kwenye mali, shirikiana naye zaidi kuliko ndugu zako, kumbuka ndugu zako nao wanatafuta kwaajili ya watoto wao ambao si wako! 


5. Ndugu zako hawajali sana tabia mbaya za mke wako bali wanaangalia maslahi yao. Kuna mambo watakuambia ni ya kweli chunguza lakini mara nyingi ukiona kelele za ndugu hasa kama una vipesa basi jua wanamuona mke wako kama atawawekea kauzibe. Usiwe mtu wa kubeba bebeba kila kitu, chunguza, kuwa karibu na wanao, ongeaongea nao utajua, binti wa kazi ongea naye na majirani, ndugu wanakua na kelele sana wakiona mke wako kawazidi kete kwenye mali zako.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad