Dirisha la usajili barani Ulaya linatarajiwa kufungwa usiku wa leo Oktoba 5 mwaka 2020, katika saa hizi chache zilizobaki mpaka sasa kila klabu ina haha kuhakikisha inakamilisha sajili ya nyota waliyokusudia kuwanasa ili kuboresha vikosi vyao.
Ikiwa na presha kubwa ya usajili Manchester United baada ya hapo jana kupokea kipigo kizito cha jumla ya magoli 6 – 1 kutoka kwa Tottenham miamba hiyo ya Premier League inatarajia kuwanasa nyota hawa ili kuepukana na kadhia hiyo ya mabao kwenye michezo yake ijayo.
Ousmane Dembele huyu ni mchezaji pekee wa mkopo ambaye amebakia kwa Manchester United kama itaamua kufanya hivyo na kutimiza masharti ya Barcelona.
Beki wa Porto, Alex Telles kwa sasa anakwenda kukamilisha vipimo vya afya akichukuliwa kwa dau la paundi milioni 15.4.
Winga wa miaka 18 kutoka Uruguay anayekipiga Penarol, Facundo Pellistri inatarajiwa kuwa tayari ameshaondoka Urugay kwa dau la paundi milioni 9 hawa wote watajiunga na Edinson Cavani ambaye pia anaelekea kwenye vipimo vya afya.
Everything you need to know about Man Utd target Facundo Pellistri - Planet Football
Winga wa miaka 18 kutoka Uruguay anayekipiga Penarol, Facundo Pellistri
Kwa mujibu wa ‘ESPN’, Manchester United imekata tamaa kabisa ya kufanikiwa kumsajili Jadon Sancho na kama endapo dili la Ousmane Dembélé litashindikana katika muda huu mchache waliyobaki nao United itamsajili winga, Kingsley Coman kutoka Bundesliga ingawaje haitakuwa raisi kwao kumtoa Coman Allianz Arena.
Taarifa nyingine ni kuwa mtukutu Super-sub Mario Balotelli huwenda akarejea tena England, mchezaji huyu aliye vitumikia vilabu vya Manchester City and Liverpool kuna dalili za kumshuhudia tena.
Klabu ya Watford ipo katika mazungumzo na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuona kama itaweza kupata huduma yake.
Muitalia huyo amepata bahati ya kuzichezea klabu za Manchester City na Liverpool na zote akazipatia ubingwa wa Premier League.