Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Bonnah Kamoli, kwa mara nyingine tena amefanikiwa kushinda nafasi ya ubunge katika jimbo la Segerea dhidi ya mpinzani wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,CHADEMA,John Mrema.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi,Bonnah Kamoli, ametangazwa kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Segerea kwa kupata kura 76,828 akifuatiwa na John Mrema wa CHADEMA aliyepata kura 27612.
Akizungumza baada ya kupata ushindi huo Kamoli amesema''Miezi miwili tumefanya kampeni za kistaarabu tumemaliza siasa sasa tunaenda kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Segerea kwa hiyo niwaombe muendelee kuniunga mkono''
Aidha amelipongeza Jeshi la polisi pamoja na Tume ya uchaguzi kwa kuhakikisha haki inatendeka na kuendesha uchaguzi wa huru na wenye amani