Marapa Matajiri Zaidi Duniani Hawa Hapa



KWA hapa Bongo, inaaminika mastaa wa wanaoimba, ndio matajiri zaidi kuliko wale wa kufokafoka (Hip Hop).


Tofauti na mtazamo huo wa Kibongo, huko Marekani wapo mastaa ambao ni wa hip Hop lakini wana utajiri wa kutisha.


Twende tukaitazame Top Five ya mastaa wa Marekani lakini pia duniani kote wanaotajwa na mitandao mbalimbali kuwa ndio wanaoongoza kwa utajiri:


KANYE WEST


Kanye West ni moja kati ya marapa bora wa muda wote. Mafanikio yake makubwa ya kwenye mitindo na fasheni ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza utajiri wake. Kingine kilichochangia mapato yake, Kanye ameachia sokoni albamu 9 ambazo karibia zote zimeuza kwa kiwango cha juu (multi-platinum).


Kanye ameuza karibu nakala milioni 100 duniani kote. Miongozi mwa dili zinazomuingizia mapato ni pamoja na ubalozi ikiwemo wa kampuni ya Adidas. Kwa ujumla, Kanye ana utajiri wa Dola Bilioni 3.2 (Shilingi Trilioni 7. 4) .


JAY Z


Mkali huyu kutoka pande za Brooklyn ambaye ni mjasiriamali ndiye rapa wa kwanza kuwa bilionea katika historia. Jamaa ameweka kibindoni Dola Bilioni 1 (Trilioni 2 .3) peke yake. Lakini ukisema uchanganye utajiri wake na wa mkewe ambaye pia ni staa wa muziki Marekani Beyonce, wanakuwa na utajiri wa Dola Bilioni 1.5 (Shilingi Trilioni 3. 4)


Utajiri wa Jay Z unatokana na uwekezaji wake katika timu za michezo, studio za kurekodia kazi za wasanii, mavazi, kumbi za starehe na mambo mengine kibao.


P DIDDY


Mkongwe huyu naye hayupo nyuma kwenye marapa ambao kimsingi wamefanikiwa kutusua kwenye suala zima la utajiri. Kwenye akaunti yake benki kunasoma Dola Milioni 885 (Shilingi Trilioni 2.5) Mwana huyu mzaliwa wa New York ana majina kama yote, unaweza kumuita Puff Daddy, Puff, Diddy au Sean Combs.


Aliunda lebo yake ya Bad Boy Entertainment mwaka 1993. Mwaka 1997 aliachia albamu yake ya No Way Out ambayo iliuza kwa nakala nyingi (platinum) zaidi ya mara saba.


Mkwanja wake pia anautengeneza kupitia ujasiriamali wa mavazi, migahawa, vileo na kampuni ya miamvuli.


DR DRE


Tofauti na marapa wenzake, mwamba huyu amejiongeza kwa kufanya vipaji vingi ikiwemo uprodyuza, uigizaji na fundi wa sauti (audio engineer). Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni kubwa ya vifaa vya muziki (Beats Electronics), Beats by Dre.


Jamaa huyu ambaye amewasaidia kwa kiasi kikubwa marapa wenzie wenye mafanikio kama vile Eminem, Snoop Dogg na marehemu 2Pac, akaunti yake benki inasoma mpunga usiopungua Dola Milioni 820 (Shilingi Trilioni 1. 9).


EMINEM


Marshall Bruce Mathers II, ndiyo jina alilopewa na wazazi wake kabla ya kujiita Eminem baada ya kujizolea mashabiki lukuki. Huyu ndiye anayekamata nafasi ya tano katika marapa wenye ukwasi wa kutosha kwani anao mpunga usiopungua Dola Milioni 230 (Shilingi Biloni 533.6)


Mafanikio yake yanatajwa kupatikana zaidi kwa kazi zake za muziki ambapo nyimbo zake zimekuwa na mafanikio makubwa sana sokoni duniani kote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad