Marekani yaionya China dhidi ya kuivamia Taiwan



Mshauri wa usalama wa taifa nchini Marekani, Robert O'Brien, ameionya China dhidi ya jaribio lolote la kuitwaa Taiwan kwa nguvu, akisema operesheni za kijeshi ya ardhini, baharini na angani huwa ngumu na kwamba kuna utata mkubwa juu ya namna Marekani itakavyojibu hatua hiyo. 

O'Brien alisema hapo jana akiwa mjini Nevada, Las Vegas, kwamba China inafanya matayarisho makubwa ya jeshi la majini ambayo yumkini hayajawahi kushuhudiwa tangu jaribio la Ujerumani kushindana na jeshi la majini la Uingereza kabla ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. 


Alisema sehemu ya matayarisho hayo ni kuwapa uwezo wa kuisukuma Marekani nje ya Pasifiki Magharibi, na kuwaruhusu kutua Taiwan katika operesheni za jeshi la ardhini, baharini na angani. 


Marekani inatakiwa kisheria kuipaTaiwan uwezo wa kujilinda, lakini haijabainisha wazi iwapo itangilia kijeshi ikiwa China itaishambulia Taiwan, jambo ambalo huenda likasababisha mzozo mpana zaidi na Beijing. 


O'Brien pia ameitolea wito Taiwan kuongeza matumizi yake ya kijeshi na kufanya mageuzi ya kijeshi, ili kuipa ujumbe wa wazi China juu ya hatari za kujaribu kuivamia. China inaitambuwa Taiwan kuwa sehemu yake iliyojitenga.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad