Mamilioni ya raia barani Ulaya jana Jumamosi walikabiliwa na vikwazo vipya vya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona huku serikali zikiimarisha juhudi za kupunguza kuongezeka kwa maambukizi baada ya shirika la afya duniani WHO kuripoti kiwango cha ”kutia wasiwasi” cha ongezeko la asilimia 44 la maambukizi barani Ulaya katika muda wa wiki moja.
France's Coronavirus Death Rate, New Cases Slow | World News | US News
Kutoka jana jioni, mji wa Paris na miji mingine ya Ufaransa iliwekwa chini ya marufuku ya kutotoka nje katika saa za usiku ambayo itadumu kwa takriban mwezi mmoja.
Uingereza imepiga marufuku mikusanyiko katika nyumba katika mji wake mkuu London pamoja na maeneo mengine huku eneo la wakazi wengi nchini Italia likithibiti kufunguliwa kwa mabaa na kuahirisha hafla za michezo.
Nchini ujerumani Kansela Angela Merkel amewatolea wito raia wa nchi hiyo kushirikiana pamoja kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona wakati ambapo nchi hiyo imetangaza idadi kubwa ya maambukizi ya siku ya COVID-19.