"Matatizo ya afya ya akili siyo wendawazimu" - Dkt



Wadau wa afya wameiasa jamii kuepuka kuwahukumu watu wenye matatizo ya afya ya akili huku wakiomba serikali kuwekeza katika mifumo na miundombinu madhubuti ya utoaji wa huduma kwa watu wenye matatizo hayo.



Wakizungumza  leo Jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam katika maadhinisho ya siku ya  Afya ya Akili Duniani, wadau wamesema jamii imekua ikiwatenga watu wenyewe matatizo ya afya ya akili wakati watu hao wakipewa huduma stahiki wanaweza kuishi katika mazingira yanaowazunguka bila hofu yoyote.


''Utoaji wa huduma ya afya ya akili katika jamii za vijijini na mijini ni muhimu kuimarishwa, watu waondoe imani za kishirikina kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili na kuacha kuwahukumu'' amesema Dkt. Rashid Mfaume Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam.


Kwa mujibu watakwimu za  Shirika la Afya Duniani (WHO) watu bilioni 1 Duniani wanaishi na matatizo ya afya ya akili,na kati ya watu wanne mmoja ana changamoto ya afya ya akili.


Ni miaka 30 imetimia toka kuanza kuadhimishwa kwa siku ya Afya ya Akili duniani .


 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad