Matumizi ya Limao Kusafisha Uke ni Hatari Kiafya



Kwa mujibu wa Dkt. Fatima Abdulahi, Daktari Bingwa wa Wanawake katika Hospitali ya Marie Stopes mjini Abuja amesema, kisayansi kila kiungo katika mwili wa binadamu kina kemikali kama vile Tindikali na Alkalini kwa kiwango kinachohitajika mwilini

Maji ya limao yanasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha Tindikali ambacho ni cha pili kwa ukubwa cha 14/1/14, wakati uke wa mwanamke una kiwango cha kati ya 3.8 / 14 na 4.5 / 14 cha Tindikali

Kuna baadhi ya wanawake wanaodaiwa kutumia Limao kujisafisha lakini wataalamu wanasema ni hatari kufanya hivyo kwasababu maji ya limao yana ukakasi wa hali ya juu ambao unabadilisha mfumo wa asilia ya uke

Matumizi ya ndimu kusafisha uke yanaweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa katika eneo hilo ikiwemo kuathiri shingo ya uzazi hali ambayo inaweza kusababisha Saratani ya Shingo ya kizazi

Wanasayansi wanashauri uangalifu uzingatiwe wakati wa kujisafisha ili kujiepusha kupata michumbuko ambayo hupelekea mwanamke kupata maradhi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad