TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekataa kuwaapisha mawakala 12 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile ilichobainisha kuwa wamefoji saini ya Katibu Mkuu wa CHADEMA wa Wilaya.
Akizungumzia suala hilo, mgombea ubunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amesema kupitia akaunti yake ya Twitter:
“Wagombea wanaambiwa mawakala wataapa kwenye tarafa nk. Hakuna ngazi ya tarafa kwenye uchaguzi. Mawakala wanapaswa kuapa ama kwa msimamizi msaidizi (kwenye kata) au kwa msimamizi wa uchaguzi (kwenye jimbo). Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wanasumbua wagombea makusudi.
“Miaka yote katika chaguzi zote mawakala wetu wanaapishwa makao makuu ya kata na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi. Leo mkurugenzi anataka tusafirishe watu zaidi ya 1,600 kwenda halmashauri maeneo mengine umbali wa km 60 kwa barabara zetu, risk, gharama na usumbufu mkubwa.
“Nimeongea na mkurugenzi wa tume Dk Mahera akasema anatoa maelekezo kwa msimamizi wa uchaguzi lakini bado msimamizi amegoma. Badala ya uchaguzi kuwa wa wadau unakuwa mali ya msimamizi ambaye alipaswa kuwa facilitator tu. Impunity, ujinga na uhuni.”