Mbunge Mteule wa Jimbo la Butiama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumanne Sagini amewaomba wananchi wa Kata ya Bwiregi kuwaogopa wanasiasa wanaoshabikia ushoga kwani maandiko matakatifu yanasema ni chukizo kwa Mungu na kupoteza uhalisia wa mwanume kamili kutoka Mkoa wa Mara.
Tunataka kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema sio kila kitu kinachofanywa na wazungu sisi waafrika tuige, na unapomsikia kiongozi wa juu hapa nchini anasema hapati taabu na ushoga wapewe haki zao huyo ni hatari katika nchi kutokana na kutengeneza vizazi visivyo na maadili.
"Kutokana na maandiko matakatifu hukumu ya ushoga ambapo Sodoma na Gomola iliunguzwa moto sasa hapa nchini mwanaume awe shoga sidhani kama hataweza kulima hata birika la chai hataweza kulibeba na viungo vitakuwa legevu kwa ufupi tutapoteza vijana wetu," amesema Sagini.
Sagini ameeleza kuwa alitegemea kuona viongozi wa wa upinzani hapa nchini wakimpongeza Rais Awamu wa Tano Dk John Magufuli kutokana na kazi za maendeleo alizofanya pia zinaonekana hasa katika sekta ya afya kajenga hospitali mpya za wilaya takriban 67 ikiwemo ya Kanda ya Kangwa ambayo haikukamilika toka awamu ya kwanza.
Aidha ameomba wananchi ifikapo tarehe 28 mwezi wa kumi mwaka huu kwenda kuwapigia kura za kishindo wagombea wote wa CCM katika nafasi za madiwani mbunge na rais ili kutekeleza na kuendeleza miradi ya maendeleo iliyokomea njiani kwa kipindi cha miaka mitano