Mbwa wa Cristian Mallocci alimuonesha mmiliki wake maajabu baada ya kuzaa mbwa asie wa kawaida.
Mbwa huyo aliyepewa jina Pistachio tofauti na dada zake na kaka zake waliokuwa na manyoya ya rangi nyeupe, mbwa huyo alikuwa wa rangi ya kijana.
Inasemekana kwamba mbwa wa aina hii huwa ni nadra sana kwasababu chanzo chake lazima mama yake alikutana na mbwa wa rangi ya kijani.
Bwana Mallocci ameamua kuuza mbwa wote isipokuwa huyo wa kipekee.
Mmiliki wa mbwa huyo anaamini kuwa rangi hiyo ya kijana ni ya matumaini na bahati nzuri jambo ambalo huenda likawa nadra mwaka huu wa 2020.