Memphis Depay akubali kujiunga na Barcelona



Mshambuliaji wa lyon na Uholanzi Memphis Depay amekubali kuingia mkataba na Barcelona na huenda akajiunga na Barcelona katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, kulingana na mkurugenzi wa Ufaransa Juninho.

Mchezaji huyo wa zamani wa man United mwenye umri wa miaka 26 aliwachwa nje katika kikosi cha timu ya kwanza ya Lyon siku ya jumapili iliuotoka sare na Marseille.


Amekubaliana na Barcelona , hilo hatuwezi kuficha hata kidogo, alisema Juninho. Wakati huohuo beki Eric garcia anaweza kujiunga tena na barcelona kutoka manchester City.


Ligi hiyo ya premia ingeruhusu kinda huyo kurudi iwapo itapokea ombi zuri , lkaini pia wamejiandaa kumwachilia raia huyo wa Uhispania kuondoka katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao.


Garcia ni mchezaji huru baada ya kandarasi yake kukamilika msimu uliopita na ameambia City kwamba hatotia saini kandarasi nyengine.


Wakati huohuo mchezaji wa Lyon Depay amefunga magoli 58 katika mechi 144 tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Ligue 1 kutoka manchester United 2017.


Depay alikuwa na wakati mgumu katika ligi ya Premia akiichezea United baada ya kusainiwa na Lousi van Gaal kwa dau la £31m mwaka 2015 , akifunga magoli 7 katika mechi 53.


Iwapo Depay atakamilisha uhamisho huo atashirikiana aliyekuwa mkufunzi wa Uholanzi Ronald Koeman , ambaye alichukua uojngozi wa barcelona msimu huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad