Mkumbo amuangusha aliyewahi kuwa Meya Ubungo

 


Mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Kitila Mkumbo, ameibuka mshindi  katika uchaguzi wa jimbo la Ubungo dhidi ya mgombea wa CHADEMA ambaye pia aliwahi kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.

 

Kushoto ni Mbunge mteule wa jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo na kulia ni aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Boniface Jacob


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi Prof. Kitila Mkumbo, amewashukuru wananchi wa Ubungo kwa kumuamini na kuahidi kwenda kusimamia kero zote zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo.

 

Na huko Iringa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Mufindi kusini mkoani Iringa John Quiman amemtangaza David Kihenzile kutoka CCM kuwa mshindi kwenye nafasi ya ubunge kwa kupata kura 59,793 sawa na asilimia 97.21

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad