Mtalii mmoja wa Kimarekani aliyekuwa akitalii Thailand ameripotiwa kutiwa mbaroni baada ya kuandika maoni yanayochafua hoteli aliyofikia.
Mmarekani huyo aitwaye Wesley Barnes ambaye ni mwalimu wa Kiingereza nchini humo,alikuwa akikaa kwenye hoteli moja ya alipokuwa akitalii.
Wesley Barnes alichapisha maoni yake kuhusu hoteli hiyo kwenye blogu yake na kumsababisha angie hatiani kwa kosa kauli za uchafuzi.
Mtalii huyo aliyelala siku mbili kwenye hoteli hiyo, aliachiliwa kwa dhamana ya fedha baht 100,0000 na kuondoshewa uamuzi wa kufikishwa mbele ya mahakama.
Polisi waliarifu kwamba Barnes aliafikiana na mamlaka ya utalii ya Thailand kwa sharti la kukubali kuomba radhi.
Kama Wesley Barnes angekutwa na hatia, basi angehukumiwa kifungo cha miaka hadi miwili.