Aliyekuwa mtia nia katika kura za maoni katika jimbo la Kongwa Samwel Chimanyi amesema,kutokana na aliyoyafanya Rais Dkt.John Magufuli ,kulikuwa hakuna haja ya kufanya uchaguzi Mkuu mwaka huu na badala yake viongozi wa vyama vyote vya siasa wangekubaliana kutosimamisha wagombea na kumpa ridhaa Dkt.Magufuli kuendelea katika kipindi cha pili cha miaka mitano.
Akizungumza jijini Dodoma Chimanyi amesema,mambo mengi ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama vya upinzani Dkt.Magufuli ameyafanya.
Amesema,kama viongozi wote wa vyama vya siasa angekubaliana Dkt.Magufuli aendelee kuongoza kumalizia kipindi chake cha miaka mitano, nchi isingeingia katika uchaguzi na ingeokoa mabilioni ya fedha ambazo zimetumika katika mchakato mzima wa uchaguzi na kupeleka katika miradi ya maendeleo.
"Licha ya kuwa ni haki yao kikatiba kusimamisha wagombea kutoka katika vyama vyao lakini wangekuwa wazalendo tu kumuunga Dkt.Magufuli mkono ili aendelee na kukamilisha mambo ambayo ameshaanza." Amesema Chimanyi.
Amesema,Dkt.Magufuli ambaye amegombea tena nafasi ya urasi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),amefanya mambo makubwa hapa nchininkwa ajili ya Maendwleo ya watanzania .
Aidha amesema,licha ya kujenga miradi mikubwa lakini pia kiongozi huyo ameweza kudhibiti rushwa nchini lakini pia kuwakabili mafisadi ambao walikuwa wakiitafuna nchi kwa kula mabilioni ya fedha za Serikali na kujinufaisha wao binafsi badala ya kuwanufaisha watanzania.
"Tuseme ukweli Dkt.Magufuli katika mambo haya amefanya kwa vitendo,Licha ya kuwa bado hayajaisha kanisa lakini akipata nafasi nyingine atayasimamia kwa nguvu na kuyapunguza kwa kiasi kikubwa kama siyo kuyamaliza kanisa." amesema.
Kufuata hali hiyo Chimanyi amewaasa watanzania kumchagua kiongozi mpenda maendeleo na mwenye uwezo wa kuwamudu hata walio chini yake.
"Ninafahamu kila mtanzania ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka,ndio maana nawasihi watumie haki hiyo vizuri kwa kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza na kuwaletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
"Pia watanzania wamchague Rais atakayeondoa mafisadi,nchi hii ilitawaliwa na rushwa na mafisadi lakini katika uongozi wa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuyapunguza haya mambo,mafisadi wamerudisha fedha nyingi za Serikali , na nina uhakika akipata ridhaa nyingine mambo hayo yanaweza kumalizika kabisa."