Muigizaji Terrence Howard ameishtaki kampuni ya 20th Century Fox kwa madai ya kuchukua picha yake toka kwenye filamu ya 'Hustle & Flow' na kuitumia kutengeneza Chapa (logo) ya filamu ya Empire.
Terrence ambaye alicheza kama Lucious Lyon kwenye misimu yote 6 ya Empire amefungua shauri hilo akidai kwamba 20th Century Fox walikuwa wakimpiga chenga pale ambapo alikuwa akiwauliza kuhusu ni wapi wameipata logo ya Empire kwani hakuwahi kufanya photoshoot.
Kwenye nyaraka zilizodakwa na TMZ, Terrence alisema aliibaini picha iliyopo kwenye logo ya Empire kuwa imechukuliwa toka kwenye filamu ya 'Hustle & Flow' ya mwaka 2005, kwenye scene iitwayo 'It's 'Hard Out Here for a Pimp.' kisha kuigeuza toka kuangalia kulia na kuielekeza sura kushoto, (Pichani juu)
Amesema angeweza kupata pesa toka kampumi ya Paramount, studio ambayo ilihusika kuitengeneza 'Hustle & Flow' kama 20th Century wangefuata utaratibu wa kuichukua picha yake na kuitumia kwenye Empire, hivyo amefungua kesi ya madai dhidi yao akidai fidia.