EATV imefika eneo maarufu kwa ukaangaji wa samaki aina ya ngisi, pweza na kadhalika Mwananyamala A na kuzungumza na takribani zaidi ya vijana thelathini ambao kwa pamoja wameamua kufanya biashara hiyo wakieleza ugumu ambao wamekutana nao kwa sasa mara baada ya kuanza kwa mvua.
Aidha, wamebainisha kuwa wao kama vijana wamelazimika kuungana ili kuhakikisha wanaacha kujihusisha na vitendo viovu huku wakiomba serikali na wadau kuwasaidia changamoto za eneo la biashara wanalofanyia kazi ili wazidi kujikwamua kiuchumi.
Bado zipo changamoto nyingi ambazo zinatajwa kuwakwamisha vijana wengi wanaoanza biashara ikiwemo kutokuwa na dhamana za wao kukopesheka.