Mvua Yaua Watu 12 Jijini Dar es Salaam



Watu kumi na wawili (12) wameripotiwa kufa kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam, na wengine watano wa familia moja wakiripotiwa kufa kutokana na ajali ya moto.


Akizunguza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa amesema, vifo hivyo vimetokea katika maeneo tofauti ya mkoa wa Kipolisi wa Wilaya ya Kinondoni na Ilala kati ya tarehe 13 na 14 Oktoba mwaka 2020.


Kufuatia tukio hilo kamanda Mambosasa amewataka wananchi kuchukua tahadhari zinazostahiki ili kuepuka majanga yatakayosababishwa na mvua.


Kuhusu ajali ya moto Kamanda Mambosasa amesema ajali hiyo iliyotokea maeneo ya Pugu nakusababisha vifo vya watu watano wa familia moja nakubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.


Hata hivyo Kamanda Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad