Mwafrika apigwa faini Ufaransa kwa kuiba sanamu ya Afrika jijini Paris



Mwanaharakati mwenye asili ya Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo ametozwa faini ya euro 1000 kwa kuondoa sanamu ya Afrika kutoka makumbusho moja ya Paris katika maandamano ya kupinga wizi wa sanaa za Afrika kulikotekelezwa enzi ya ukoloni yanayolenga Ufaransa.


Congo-born Emery Mwazulu Diyabanza speaks to reporters after the verdict at the Paris Palace of Justice, October 14, 2020 [Lewis Joly/AP]


Emery Mwazulu Diyabanza alichukua sanamu ya mbao ya karne ya 19 kutoka makumbusho ya Quai Branly mnamo mwezi Juni katika maandamano yaliyooneshwa moja kwa moja kwa njia ya mtandao.


Alisema “Nimekuja kuchukua kilichoibwa Afrika”. Akimtoza faini kubwa kwa wizi, hakimu alisema anataka kumaliza tabia za aina hiyo.


“Kuna njia zingine unazoweza kutumia kuvutia wanasiasa na umma” kuhusu suala la wizi wa vitu vya kale vilivyochukuliwa wakati wa ukoloni, jaji alisema.


Wanaharakati wengine watatu walioungana na Diyabanza katika makumbusho walipigwa faini ya euro 250, 750, na 1,000, kila mmoja, kulingana na shirika la habari la AFP huku wa nne alifutiwa mashtaka.




Katika video ya nusu saa iliyowekwa kwenye mtandao wa Youtube, Diyabanza anaonekana akichukua kinyago kutoka sehemu ilipowekwa. Yeye pamoja na wanaharakati wengine wakaibeba huku wakipaza sauti na kusema “tunaipeleka nyumbani” lakini wanazuiwa na walinzi kuondoka kwenye makumbusho hiyo.


Diyabanza, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekuwa akishiriki maandamano ya aina hiyo katika miji mingine ya Ufaransa na Uholanzi.


Mwezi uliopita aliliambia gazeti la New York Times: “Ukweli wa kwamba nahitajika kulipa pesa yangu kuona kile kilichochukuliwa kwa nguvu, urithi huu ambao ni wa nyumbani ninakotoka – hapo ndio nilifikia uamuzi wa kuchukua hatua.”


Alielezea makumbusho ya Quai Branly “kama yenye sanaa za kuibwa”. Sanamu aliyochukua inasemekana kwamba ilikuwa ni zawadi kutoka kwa daktari wa Ufaransa.


Ripoti iliyozinduliwa na Rais Macron mwaka 2018 ilihesabu bidhaa za sanaa 90,000 za Afrika, nyingi zikiwa ni bidhaa za kale kutoka eneo la jangwa la Sahara barani Afrika.Screen grab of Emery Mwazulu Diyabanza grabbing the funerary post


Wanaharakati walirekodi tukio la wao kuchukua sanamu wanayodai iliibwa Afrika

Wiki iliyopita, mawakili wa Ufaransa walipiga kura kuregesha baadhi ya vitu vya kale hadi Benin na Senegal zilizochukuliwa wakati wa enzi za ukoloni ambazo zinaoneshwa katika makumbusho ya Paris.


Vitu hivyo vya kale ikiwa ni pamoja na kiti cha enzi cha Mfalme Glele wa Benin na upanga ambavyo kuna wakati vilisemekana kuwa vya mwanajeshi wa Senegal aliyekuwa karibu sana na dini, Omar Saidou Tall.


Ufaransa sio nchi pekee inayokabiliwa na maandamano ya kupinga bidhaa za kale zilizoibwa wakati wa ukoloni.


Uingereza, mwanaume wa miaka 33, Isaiah Ogundele, alipatikana na hatia licha ya kutokuwepo mahakama mwezi uliopita kwa tabia ya kutishia wengine wakati wa maandamano katika Makumbusho ya London yenye kuhusishwa na nyakati za utumwa baada ya kusemekana kwamba alichukua kazi za sanaa za kale kutoka kwenye maeneo zilipowekwa katika makumbusho hiyo.


Kulinga na gazeti la New York Times, wakati wa mahojiano na Bwana Diyabanza, alidai kuwa akiwa kijana kule kuliko fahamika kama Zaire, anasema mama yake alimwambia kwamba karne ya 19, wakoloni wa Ulaya walichukua vitu vitatu muhimu – fimbo iliyochongwa, ngozi ya chui na bangili – kutoka kwa babu yake, aliyekuwa gavana wa Congo ambaye alikuwa amepokea baadhi ya vitu kama ishara ya madaraka na mamlaka kutoka kwa mfalme wa nchi.


“Urithi huu ulichukuliwa kwa nguvu,” Bwana. Diyabanza alisema.


“Nilichosikia kutoka kwa mama yangu kilichangia katika fikra zangu, na kilinipa nguvu na hamasa ya kuhakikisha urithi huu, siku moja umerejea nyumbani.”


Diyabanza anasema imemchukua miaka mingi kutafuta bidhaa hizo na ana amini kwamba amefanikiwa kuona baadhi tu ya bidhaa hizo za kale katika makumbusho mbalimbali kote duniani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad