Mwandishi wa habari aomba radhi kwa kumfananisha mchezaji wa Barcelona na 'mchuuzi mweusi wa barabarani'



Mwandishi wa habari wa Uhispania ameomba msamaha baada ya kumlinganisha Ansu Fati wa Barcelona na mchuuzi mweusi wa barabarani kwenye mechi iliyowapa ushindi wa 5-1 wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ferencvaros.


Fati, 17, alifunga mabao kwenye mechi ya Jumanne na aliungwa mkono na mwenzake Antoine Griezmann kwenye mtandao wa Twitter.


Griezmann alisema: "Ansu ni kijana wa kipekee anayestahili heshima kama binadamu yeyote. napinga ubaguzi wa rangi.''


Fati ni mchezaji wa kwanza wa chini ya miaka 18 kushinda magoli mawili ya Champions League


Ripoti ya mechi ya Salvador Sostres katika gazeti la Uhispania ABC ilimfananisha winga wa Uhispania na "mchuuzi mweusi wa barabarani" ambaye "unamuona ghafla akikimbia" polisi wanapowasili.


Katika ombi la msamaha lililochapishwa na ABC mnamo Alhamisi, Sostres alisema kwamba alikuwa akijaribu "kusifu uzuri wa harakati za Ansu" na alikuwa "na aliomba radhi kwa namna alivyoeleweka vibaya''.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad