Ndege za kivita zagongana, tisa wafariki



Ajali ya ndege mbili za kijeshi aina ya helkopta za Afghanistan zimesababisha wanajeshi kujeruhiwa huko kusini mwa jimbo la Helmand na wengine tisa kufariki.


An Afghan Army helicopter takes off from a military base after Taliban launched first large-scale attack on the capital of southwestern Helmand province in Afghanistan since the signing of a peace deal with the United States in late February, in Lashkargah, Helmand, Afghanistan, 14 October 2020.


Wote waliofariki walikuwa ndani ya ndege hizo, maofisa wamesema.


Tukio hilo limetokea mapema Jumatano katika kitongoji cha Nawa na ajali hiyo ilisababishwa na tatizo la kiufundi.


Eneo hilo limekuwa na mapigano hivi karibuni kati ya Taliban na jeshi la serikali ya Afghanistan , wakiungwa mkono na wanajeshi wa angani kutoka Marekani.


Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea pembezoni mwa mji wa Lashkar Gah ambako kulikuwa tayari kumedhibitiwa


Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu 35,000 wamelazimika kuhama makazi yao huko Helmand.Afghan security officials patrol on Helmand-Kandahar highway after Taliban launched first large-scale attack on the capital of southwestern Helmand province in Afghanistan since the signing of a peace deal with the United States in late February, in Lashkargah, Helmand, Afghanistan, 13 October 2020.


Jeshi la Afghan likiwa Helmand-Kandahar likipigana na Taliban

Hili ni shambulio kubwa zaidi la Taliban kutokea na kuchukua muda mrefu. Mwezi uliopita majadiliano ya amani yalianza.


Mpaka sasa majadiliano yanakaribia kumaliza kutengeneza sheria na mchakato wa majadiliano hayo ambayo yanahusiana na kusitisha kwa ghasia na namna ya kushirikiana katika mamlaka.


Mapema wiki hii kiongozi wa jeshi la Nato nchini Afghanistan, Generali wa Marekani Scott Miller, amelaani kitendo cha Taliban kupuuzia mazungumzo hayo ya amani na hata kukiuka makubaliano waliyosaini mwezi Februari.


Sehemu kubwa ya Helmand na jirani yake Kandahar zimesalia bila umeme baada ya shambulio la Taliban lililozima umeme Jumatatu.


Baadhi ya miundo mbinu ya mawasiliano ilizimwa pia.


Zaidi ya familia zipatazo 5,000 zimehama makazi yao na hazijulikani zilipo, baadhi ya taarifa zinasema walihamia maeneo ya nchi jirani.Afghans flee their villages after fighting intensified between Taliban militants and security forces, in Lashkar Gah, the provincial capital of restive Helmand province, Afghanistan, 12 October 2020


Familia moja iliiambia BBC kuwa iliondoka nyumbani kwao huko Lashkar Gah ikiwa na nguo alizovaa pekee, bila kujua ni wapi itapata eneo salama la kulala.


Wengine walisema walikuwa wanaogopa kuwa watakufa na njaa, wakati watoa huduma wa hospitalini walisema wana wagonjwa wengi.


Mazungumzo ya amani yalianza Septemba 12, siku moja baada ya kumbukumbu za shambulio kubwa la l-Qaeda lililotokea Septemba 11 kwa ofisi za Marekani , ambalo lilisababisha Marekani kuanza operesheni ya kijeshi Afghanistan.


Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi wa Afghan kukaa meza moja na wanamgambo wa makundi ya Kiisalamu.


Lakini kitendo cha Taliban kukubali kilizua maswali mengi juu ya nia yake.


Jeshi limesema linachukua maeneo yale tu yaliyokuwa imeyathibiti.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad