Nigeria kufungua shule Oktoba 12



Shule nchini Nigeria zinatarajiwa kufunguliwa mnamo Oktoba 12, kufuatia kupunguwa kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo kama ilivyotangazwa na wizara ya afya hapo jana.

 Taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, lilifunga shule mnamo mwezi Machi, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.


 Idadi ya maambukizi mapya ya virusi hivyo imeshuka hadi wagonjwa 200 kwa siku, ikilinganishwa na maambukizi yapatayo 700 yaliyokuwa yakiripotiwa katika miezi ya Julai na Agosti. 


Tangazo hilo limetolewa sambamba na ushauri unazozitaka shule zote za serikali na za binafsi kufuata kwa makini miongozo ya usalama wa afya ya COVID-19.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad