Nigeria yavunjilia mbali kikosi maalum cha polisi baada ya maandamano



Nigeria imevunjilia mbali kikosi chake maalum cha polisi baada ya maandamano ya umma kutokana na madai ya ukatili wa polisi na itafanya uchunguzi kuhusu shughuli za kikosi hicho. Hayo yametangazwa leo na ofisi ya urais nchini humo. 



Ujumbe wa ofisi hiyo kupitia mtandao twitter, unasema kuwa kikosi maalumu cha kukabiliana na waporaji kinachojulikana kama SARS kimevunjiliwa mbali mara moja. 




Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, jeshi la polisi nchini humo limetangaza kufanya uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu uliotendwa dhidi ya raia na kuongeza kuwa waliohusika watachukuliwa hatua. 




Awali huku maandamano hayo yakitarajiwa kuwa ya amani, waandamanaji walishambulia kituo cha polisi na kusababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi. Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi na pia kuwarushia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji hao ambao waliwashtumu maafisa hao kwa kutumia risasi za moto.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad