Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Njombe,imetoa rai kwa wananchi kuchagua viongozi wapenda haki amani,maendeleo na watakao weza kukemea vitendo vya rushwa bila kuona aibu.
Wito umetolewa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Kassim Ephrem wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Septemba,2020.
"Tunaamini tukishiriki kikamilifu katika swala la uchaguzi,tukachagua viongozi waadilifu,wanaoweza kusimama na kukemea rushwa ni dhahiri tutapeleka taifa letu katika mazingira mazuri" alisema Mkuu wa takukuru
Vile vile amehimiza wananchi kujitokeza kupiga kura"Tunahimiza wananchi tarehe 28 iko karibu,tujitokeza kwenye uchaguzi na tuchagua viongozi tunaoona wanatufaa na kuletea maendeleo.Maendeleo ya nchi yetu yanatia moyo"Kassim Ephrem Mkuu wa takukuru mkoa wa Njombe
"Kipindi hiki kilichobaki kila mmoja aangalie kadi yake ya kupiga kura iko wapi ili tarehe 28 mapema,uchague kiongozi atakayetea haki zako na hasa kiongozi atakayeweza kukemea rushwa"Kassim Ephrem
Aidha amesema TAKUKURU ikishirikiana na na vyombo vingine vya ulinzi na usalama,imeendelea na zoezi la ufuatiliaji na ukusabyaji wa fedha zilizokopwa na kufanyiwa ubadhirifu kutoka AMCOS,SACCOS pamoja na benki ya wananchi Njombe (NJOCOBA)
"Kuanzia tarehe 12/08/2020 hadi 30/09,TAKUKURU mkoa wa Njombe imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 143,557,241 kutoka AMCOS na SACCOS na shilingi 32,515,882/=kutoka NJOCOBA na kufanya jumla ya shilingi 176,073123/= "Kassim Ephrem
Katika hatua nyingine amesema katika kipindi hicho wameendelea kufanya ufuatiliaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
"Tumefanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu ambapo tulikagua ujenzi wa madarasa,vyoo na nyumba za walimu katika shule za msingi na sekondari wilaya za Makete,Wanging'ombe,Makambako na Ludewa"Kassim Ephrem
Hata hivyo amesema taasisi hiyo bado inaendelea kutoa elimu dhidi ya vitendo vya rushwa pamoja na mambo mengine ikiwemo kuelekea siku ya uchaguzi.
"Kwa kipindi cha mwezi Julai hadi septemba 2020 tumefanya uelimishaji kwa makundi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba,wanachama wa vyama vya msingi na ushirika,pamoja na mabaraza ya ardhi"alisema Kassim Ephrem Mkuu wa takukuru mkoa wa Njombe