Nyota wa filamu duniani, raia wa Kenya mwanadada Lupita Nyong’o aliyekwenda jijini Lagos, Nigeria mwezi Februari mwaka huu kwa maandalizi ya tamthilia maarufu inayotokana na riwaya iliyoandikwa na Chimamanda Adichie iitwayo ‘Americanah’ amejitoa kwenye tamthilia hiyo.
Nyong’o alivutiwa na riwaya hiyo tangu alipoisoma mwaka 2013 na alipanga kutengeneza filamu kutokana na riwaya hiyo.
Habari zimesema kuvurugika kwa ratiba kutokana na janga la COVID-19 duniani ni sababu ya kujitoa kwake.
Mbali na hilo, kwa sasa Lupita anafanya vizuri kupitia kitabu chake kipya kiitwacho ‘SULWE’ ambacho kimepata mapokezi mazuri kwa Mashabiki wake kwa kuwagusa namna alivyoweza kutoa Lugha tatu za matoleo yake. Kitabu hicho kinapatikana nchini Kenya kwa matoleo ya Lugha ya Kiswahili, Kingereza na Kijaluo.