Papa 'Aashiria Kuunga Mkono' ndoa za Watu wa Jinsia Moja

 


Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kwamba anafikiria wapenzi wa jinsia wanastahili kuruhusiwa "kuoana".

 

Wachambuzi wanasema kauli yake hiyo imeashiria wazi msimamo wake kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja, katika makala yaliyoelekezwa na Evgeny Afineevsky.

 

"Watu wanaoshirika mapenzi ya jinsi amoja wana haki ya kuwa na familia,"alisema katika filamu, ambayoilioneshwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

 

"Ni watoto wa Mungu nawana haki ya kuwa na familia. Hakuna mtu anayestahili kutengwa ama kufanywa ajihisi mnyonge kwa kuamua kuwa katika uhusiano wa aina hiyo.

 

"Tunachopaswa kuunda ni sheria ya umoja wa kiraia. ili kuwalinda kisheria."

 

Ameongeza kwamba "aliunga mkono wazo hilo", akiashiria nyakati alipokuwa Askofu mkuu wa Buenos Aires, akisema japo alipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja katika sheria, aliunga mkono ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja.

 

Filamu ya Francesco, inayoangazi amaisha na kazi ya Papa Francis, ilioneshwa kama sehemu ya Tamasha la Filamu la Roma.

 

Japo kauli ya Papa kuhusu ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja iliangaziwa, filamu hiyo pia inamuonyesha akiwahimiza wanaume wawili mashoga kuhudhuria kanisa na watoto wao watatu.

 

Muandishi wa Biografia ya Papa Francis, Austen Ivereigh, ameiambia BBC kwamba "hakushangazwa" na kauli hiyo ya hivi punde.

 

"Huo ulikuwa msimamo wake alipokuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires," alisema Bw. Ivereigh. "Siku zote alikuwa akipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja. Lakini aliamini kanisa linapaswa kutetea sheria ya kuwalinda wapenzi wa jinsia."

 

Chini ya mafundisho ya sasa ya Katoliki, uhusiano wa wapenzi wajinsia moja unaangaziwa kama "tabia potofu"

 

Mwaka 2003, shirika la mafundisho la Vatican, Usharika wa Mafundisho ya Imani, lilisema kwamba "heshima kwa watu wa jinsia moja haiwezi kwa njia yoyote kuidhinisha ya uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja au kutambuliwa kisheria kwa vyama vya wapenzi wa njinsia moja".

 

Msimamo uliopita wa Papa kuhusu mapenzi ya jinsia moja ulikuwa upi?

 

Tamko la Papa la hivi karibuni ni msururu wa maoni ambayo ametoa kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja - akiangazia msaada wanaostahili kupewa, lakini hajaidhinsha moja kwa moja mahusiano ya kimapenzi ya aina hiyo.

 

Mwaka 2013, katika kitabu cha Heaven and Earth, Papa alisema kuwa kusawazisha kisheria mahusiano ya jinsia moja na ndoa za jinsia moja itakuwa "upungufu wa kianthropolojia".

 

Pia alisema ikiwa wanandoa wa jinsia moja wataruhusiwa kuasili, "watoto huenda wakaathitika ... kwami kila mtu anahitaji kuwa na baba wa kiume na mama wa kike ambao wanaweza kuwasaidia utambulisho wao''.

 

Mwaka huo huo,alisisitiza msimamo wa Kanisa kwamba vitendo vya ushoga ni dhambi, lakini akasema mwelekeo wa ushoga sio.

 

"Ikiwa mtu anashiriki mapenzi ya jinsia moja na anamtafuta Mungu kwa nia njema, mimi ni nani nimhukumu?,"aliuliza.

 

Mwaka 2014 iliripotiwa kuwa Papa Francis aliashiria kuunga mkono ndoa ya wapenzi wa wa jinsia moja katika mahojiano, lakini ofisi yake ya mawasiliano ilikanusha taarifa hizo.

 

Na mwaka 2018, Papa Francis alisema "ana hofu" kuhusu mapenzi ya jinsia moja miongoni mwa makasisi akiongeza kwamba ni "jambo zito".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad