Passport za Cyprus, Malta zazua utata Ulaya

 


Umoja wa Ulaya umeanzisha hatua za kisheria dhidi ya Cyprus na Malta kuhusiana na mifumo tata ya ‘Passport’ ya dhahabu ya mataifa hayo kwa ajili ya wawekezaji matajiri, ukisema ilikuwa haramu na ilidhoofisha mfumo wa uraia wa Umoja wa Ulaya.



Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeziandikia barua nchi hizo, zilizojiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004, kutaka maelezo, na kuonya kwamba mifumo hiyo iliongeza hatari ya utakatishaji fedha, ukwepaji kodi na rushwa.

‘Passport’ za mataifa ya Umoja wa Ulaya zinathaminiwa sana, kwa sababu zinawapa wamiliki wake haki ya kusafiri, kuishi na kufanya kazi kwa uhuru katika nchi 27 wanachama wa kanda hiyo – haki ambayo halmashauri kuu imesema inapaswa kulindwa.

A rally in Cyprus this month protesting the practice of granting “golden passports.” Since the island began its current program in 2013, it has issued about 4,000 such documents, raising about $8.2 billion in revenue.

Cyprus tayari imesema itasitisha mfumo wake mwezi ujao, kufuatia uchunguzi wa kituo cha Aljazeera kubainisha kwamba watu kadhaa walioomba walikuwa chini ya uchunguzi wa uhalifu, vikwazo vya kimataifa au hata kutumikia vifungo vya gerezani.

Msemaji wa halmashauri kuu ya Ulaya Christina Wigand, amesema Umoja wa Ulaya umetiwa wasiwasi na miito ya Cyprus kuanzisha tena mpango sawa – na ukweli kwamba Malta imetoa taarifa kwamba inanuwia kurefusha mpango wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad