Polisi nchini Nigeria yaagiza uhamasishaji baada ya ghasia

 


Inspekta jenarali wa polisi nchini Nigeria M.A Adamu ameagiza uhamasishaji wa haraka wa maafisa wote wa polisi ili "kurudishanafasi ya umma kutoka kwa wahalifu wanaojisingizia kuwa waandamanaji'' baada ya siku za maandamano ya amani dhidi ya dhuluma za polisi na kishamachafuko ya vurugu ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu 69. 

Agizo hilo la polisi huenda likachochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini humo katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea katika muda wa miaka kadhaa. 


Katika taarifa, Adamu aliwaagiza maafisa wenzake wa polisi kudhibiti nafasi ya umma akisema ghasia zilizoko zimetosha.


Siku ya Jumanne jioni raia wa Nigeria walitazama kwa hofu wakati wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya waandamanaji wa amani wengi wao wakiwa vijana waliokuwa wakiimba wimbo wa taifa jijini Lagos, huku ripoti ya shirika la Amnesty International ikisema kuwa angalau watu 12 waliuawa. 


Matukio nchini Nigeria yamefananishwa na vuguvugu la ''maisha ya watu weusi ni muhimu'' nchini Marekani na ufyatuaji risasi wa wanajeshi umeibua shtuma za kimataifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad