Majeshi ya Azerbaijan na ya jamii ya Waarmenia leo hii yamekabiliana katika maeneo kadhaa ya Nagorno-Karabakh, ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya amani kuhusu mzozo huo huko mjini Washington, yenye shabaha ya kuufikisha mwisho mzozo huo mbaya wa eneo hilo lililozungukwa na milima, ambao umedumu kwa robo karne sasa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amepangiwa kukutana mawaziri wa Azerbaijan na Armenia katika jitihada mpya za kukomesha umwagaji damu uliodumu karibu mwezi mzima, ambao Rais Vladimir Putin wa Urusi alisema takribani watu 5,000 huenda wameuwawa.