‘PROPHET’ ambaye ni Bushiri kiongozi wa kanisa la Enlightened Christian Gathering na mkewe wamefikishwa Mahakama maalum ya uhalifu wa kibiashara Jijiji Pretoria nchini Afrika Kusini Jumatano ya jana, Oktoba 21, 2020.
Hartua hiyo imefuatia baada ya kutiwa mbaroni hapo jana Jumanne kwa tuhuma za utakatishaji fedha kiasi cha Randi Milioni 102 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya Bilioni 14.
Bushiri na mkewe walikamatwa nyumbani kwao baada ya kudaiwa kujaribu kuikwepa timu maalum ya Hawks iliyokuwa ikiwasaka, hivyo baada ya kukamatwa waliongozana na timu hiyo kuelekea kituo cha polisi cha Silverton na kikundi cha mawakili wao, amesema Msemaji wa Hawks Kanali Katlego Mogale.
Taarifa ya kanisa la Enlightened Christian Gathering ambayo ilitolewa kabla ya kukamatwa, inasema kwamba waliarifiwa na Mawakili wa Bushiri siku ya Jumatatu Alasiri kuwa Hawks waliomba kiongozi wao afike katika ofisi zao kuhusiana na uwekezaji wake unaohusiana na kampuni inayoitwa Rising Estatem.
Hii ni kesi ya pili ya utakatishaji fedha ambayo eerikali inafuatilia dhidi ya Prophet ambaye anayetajwa kuwa miongoni wa Wachungaji tajiri zaidi wa Bara la Afrika.