Rais Donald Trump alifanya kampeni kwa mwendo wa kasi jana katika ziara katika majimbo matatu kuanzia mkutano wa Michigan ambapo alimwita mpinzani wake Joe Biden "mhalifu" na kutoa mada kuwa wafuasi wa chama cha Democratic wanaipinga Marekani.
Akihutubia mkutano huko Muskegon, Michigan, Trump alizingatia mada za vita vya utamaduni wa Marekani na kuuambia umati mkubwa ulioshangilia kwamba wanademokratic wanataka "kufuta historia ya Marekani, kuondoa maadili ya Marekani na kuharibu mfumo wa maisha ya Marekani.
Trump aliimarisha juhudi zake za kumchafulia sifa Biden kama mtu fisadi na kuendeleza nadharia ya njama iliyopelekea kufunguliwa kwake mashtaka mwaka jana na ripoti mpya katika gazeti la New York inayokusudia kufichua ushahidi wa ufisadi uliofanywa na mwanawe wa kiuma Biden, Hunter.Baadaye alisafiri kwenda katika jimbo la Wisconsin eneo lenye mripuko mpya wa maambukizi ya virusi vya corona na kumalizia siku katika jimbo la Las Vegas , Nevada ambapo ataandaa mkutano mwingine katika eneo la Carson city hii leo.