RAIS Donald Trump wa Marekani amesema yupo tayari kuachia madaraka baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, kama mshindi halali atapatikana kuanzia kwenye kampeni zinazoendelea na uchaguzi.
Mgombea huyo wa chama cha Republican amesema, anasikitishwa na maswali na mijadala inayoendelea kuwa yupo tayari kuachia madaraka kwa amani, amejibu hoja hiyo na kuwa kuwa yupo tayari kuachia madaraka kama kila kitu kitaenda sawa kama mihimili mingine itaacha kumsaidia mgombea urais kupitia chama cha Democratic, Joe Biden, ambaye alikuwa makamu wa rais wa Barack Obama.
Aidha Rais Trump amemlaumu moja kwa moja Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Marekani (FBI), Christopher Wray, kuwa msaliti kwa kuruhusu majasusi wake kuchunguza kama kuna udanganyifu wowote uliotokea kwenye uchaguzi uliopita ambao alishinda na kuingia madarakani.
“Nimeshaona viashiria vingi vinavyoonyesha kumuunga mkono mgombea wa Democrats; majasusi wa serikali ya Obama bado wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha sirudi tena kwenye Ikulu ya White House, nafikiri mkuu wa FBI hafanyi kazi vizuri,” Trump aliongeza.
Uchaguzi mkuu wa taifa hilo umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, nz Trump atakuwa na kibarua cha kutetea kiti chake mbele ya mgombea wa Democratic, Joe Biden.