Rais wa Belarus “anayemgusa Askari au Mwanajeshi angalau aondoke bila mikono”



Wakati mamia ya wananchi wakiandamana kushinikiza ajiuzulu, Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko amesema yeyote anayemgusa Askari au Mwanajeshi angalau aondoke bila mikono.

Wanafunzi, Wafanyakazi wa Viwandani na Wastaafu wametikia wito wa Kiongozi wa upinzani, Sviatlana Tsikhanouskaya na kugoma ili kumlazimisha Rais Lukashenko kufanya Uchaguzi mpya kufuatia miezi ya maandamano.


Belarus imeingia katika mgogorowa kisiasa baada ya Rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 26 kutuhumiwa kuiba kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika. Hata hivyo, amekanusha mashtaka hayo na kuendelea kubaki madarakani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad