Rais wa Kyrgyzstan yuko tayari kujiuzulu



Rais wa Kyrgystan Sooronbai Jeenbekov amesema yuko tayari kujiuzulu mara tu baraza jipya la mawaziri litakapoteuliwa, wakati ombwe la madaraka nchini humo likiilazimu Urusi kuzungumzia wajibu wake ili kuhakikisha utulivu. 

Kyrgyzstan, ambayo inapakana na China na ina kituo cha jeshi la anga la Urusi, imekumbwa na machafuko tangu wafuasi wa upinzani walipoyakamata majengo ya serikali Jumanne wiki hii. 



Makundi ya upinzani, ambayo yanayawakilisha maslahi ya kikabila na koo mbalimbali, yamepiga hatua ya kwanza kuelekea kuleta utulivu, na kuongeza matumaini ya kumalizika kwa mgogoro huo ambao umetishia uzalishaji wa madini ya dhahabu nchini humo. 


Urusi imeielezea hali hiyo kuwa ya "fujo na machafuko". Urusi inajaribu kuzishawishi siasa za nchi zilizokuwa sehemu ya muungano wa kisovieti, huku mapigano yakiendelea kati ya Armenia na Azerbaijan na mshirika wa karibu wa Urusi, Belarus, inayogubikwa na maandamano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad