Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema wamejipanga kukabiliana na Vijana 150 ambao amedai wameandaliwa kila Kata na Vyama vya upinzani ili kufanya vurugu kwenye Vituo
Amesema "Inasemekana kuna baadhi ya Vijana 150 ambao watakuwa wanazunguka na bodaboda kwenye Vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kutisha wapiga kura na kuufanya Mji uonekana hauna amani. Niwaombe Wananchi amkeni Alfajiri mkapige kura na mkimaliza mrudi nyumbani"
Amesema wanazo taarifa za makundi hayo kupanga njama za kuandamana, kufunga barabara na kuwafanyia vurugu Wasimamizi. Amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura na kutokubali kubaki Vituoni akidai kulinda kura sio jukumu lao