RC DSM atoa onyo kwa watakaotaka kuvuruga amani



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya vurugu na kusema kuwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani kwenye mkoa huo atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria.



RC Kunenge, ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 31, 2020, wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa shirika la uwakala wa Meli Tanzania, na kuongeza kuwa kwa kuwa hali ya usalama ndani ya jiji hilo ni shwari, hivyo asitokee yeyote atakayevuruga hali hiyo.




"Tumeona hali ni shwari, tumemaliza kupiga kura na washindi wametangazwa, kwahiyo kwa lugha inayotumika sasa ni kuwa Dar es Salaam ni ya kijani, naomba tuendelee kuwa watulivu, serikali imejipanga na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri, ila yeyote ambaye ataonekana kuhatarisha usalama au atakayefanya matendo yatakayopelekea kuvunjika kwa amani hatutamvumilia aache Jiji letu liendelee kuwa na amani", amesema RC Kunenge.




Wakati huohuo RC Kunenge, ametembelea ujenzi wa stand mpya ya mabasi ya Mbezi Louis na kukuta ujenzi huo ukiwa katika hatua ya upauaji ambapo amemuelekeza mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Novemba 30 kama Rais MagufuliValivyoelekeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad