Official DJ wa msanii wa muziki wa bongo fleva @diamondplatnumz @romyjons ameizungumzia Album yake ya Changes lakini pia kuhusu Diamond kuhojiwa na Grammy
@romyjons ameeleza kuwa @diamondplatnumz anastahili yote hayo ingawa kuna watu wana mchukulia poa sana na ipo siku watakuja kuujua umuhimu wa Diamond katika muziki wa Tanzania.
Romy ameongeza kuwa “Watu wanamchukulia poa Sijui kwa sababu wapo nae muda wote au kwa sababu kazaliwa Tanzania ndio maana hawajui umuhimu wake? au kwa sababu ni mshikaji sana ingawa kuna watu wa karibu wanajua kabisa huyu jamaa ni mtu mwingine”
Romy ameongeza kuwa kuna wakati anaumia sana anapoona watu wakimtukana na mambo mengine lakini hana namna kwa sababu hawezi kukataza watu kumuongelea Diamond vibaya kwenye mitandao
Pia kuhusu Album yake ya Changes amefunguka baadhi ya changamoto alizopitia hadi kuikamilisha album hiyo.