Rusesabagina Anyimwa Dhamana Mahakama Rwanda



Mahakama ya juu mjini Kigali jana imekataa ombi la dhamana la Paul Rusesabagina, ikiagiza abaki kizuizini ili ashtakiwe kwa kuhusika na vitendo kadhaa ikiwa ni pamoja na ugaidi. 

Rusesabagina amekuwa akiishi uhamishoni kwa miaka mingi na alikua mkosoaji mkubwa wa serikali Rwanda. 


Lakini mnamo Agosti ghafla alijikuta amefikishwa mjini Kigali baada ya kukamatwa katika mazingira ya kutatanisha, na familia yake inadai alitekwa nyara na kupelekwa Rwanda. 


Lazima ajibu mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na ugaidi, ufadhili na kuanzisha vikundi vya wanamgambo, mauaji, uchomaji moto na njama ya kuhusisha watoto katika vikundi vyenye silaha wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. 


Uamuzi huo umetolewa na mahakama baada ya Rusesabagina mwenye umri wa miaka 66 kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa awali wa kunyimwa dhamana, akitaja sababu za kiafya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad