Chama Cha Mapinduzi kama Chama chenye kujali Utu na Maisha ya Watu, kinatoa Pole kwa familia za Watu wote waliopoteza maisha na wote walioathirika na Janga la mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam. CCM inawaahidi wananchi wa Dar es Salaam na Watanzania wote nchini kwamba kitaendelea kusimamia na kuboresha maisha ya watu wote kwa Ustawi wa Taifa letu.
#KuraKwaMagufuli2020
#T2020JPM